Jamii imetakiwa kuachana na imani za kishirikina zinazopelekea
uvunjifu wa amani na badala yake waelekeze imani yao kwa mwenyezi mungu hali
itakayo wawezesha kuishi kwa amani na upendo.
Hayo yamesemwa na Askofu mkuu wa kanisa la methodist kanda ya
afrika mashariki na kati Joseph Ntombura kupitia mafundisho yake aliyoyatoa
kwenye mkutano maalum wa injili uliofanyikia mjini Bunda.
Askofu Ntombura amesema kama jamii itamwelekea Mungu vitendo viovu kama vile rushwa na ubadhirifu
uliokithiri vitatoweka na hivyo wengi wao kufanya mambo yenye tija kwa makuzi
ya uchumi wa taifa.
Aidha Askofu Ntombura
ametumia furusa hiyo kuendesha huduma
maalum ya kumuombea Rais Dkt.John Pombe Magufuli ili azidishiwe busara na
hekima katika utendaji kazi wake wa kuliongoza vema taifa la Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni