Uongozi wa halmashauri wa wilaya ya
Butiama mkoani Mara umemsimamisha kazi daktari mwandamizi wa
hospitali wa Wilaya hiyo na kutoa onyo kali kwa mtaalam mmoja wa
maabara baada ya kudaiwa kufanya kazi kwa uzembe hatua ambayo
imesababisha kifo cha mtoto Stephen Julius mwenye umri wa miaka minne
mkazi wa kijiji cha Butiama.
Kusimamishwa kwa daktari huyo Dk Henri Japhat Msusa kunafuatia
tume iliyoundwa na uongozi wa hospitali hiyo muda mfupi tu baada ya
mtoto huyo afariki dunia na maelezo ya uzuni na kina ambayo yametolewa
na mama mzazi wa mtoto huyo Bi.Pilly Juma James, mbele ya mkuu wa mkoa
wa Mara Bw Magesa Mulongo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika
kijijini Butiama.
Akitoa taarifa ya uchunguzi wa tume iliyoundwa na uongozi wa
hospitali hiyo ya Butiama na sababu ambazo zimesababisha kifo cha mtoto
huyo,Mganga Mkuu wa halmashauri ya Butiama Dk Archard Rwezahura,
amesema mbali na mtoto huyo kusumbuliwa na malaria kali,lakini uzumbe
ambao umefanywa na watumishi hao umechangia kifo cha kijana huyo kwa
kushindwa kumpa huduma kwa zaidi ya saa nane tangu alipofikishwa katika
hospitali hiyo.
Kufutia taarifa hiyo ya uchunguzi ambao umefanywa na timu ya
madaktari wa hospitali hiyo,mkuu huyo wa mkoa wa mara Bw Magesa
Mulongo,amemuagiza mkuu wa wilaya ya Butiama kufikisha taarifa hiyo kwa
jeshi la polisi na TAKUKURU ili uchunguzi wa kina ufanyike na endapo
itabainika watumishi hao walifanya uzembe na kusabisha kifo, hatua kali
za kisheria zikuliwe dhidi ya watumishi hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni