Jumanne, 31 Mei 2016

MIRUMBE AFANIKISHA KUCHANGISHA JUMLA YA MADAWATI 326 KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA.

Halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara imefanikiwa kupunguza upungufu wa madawati kutoka 4728 hadi kufikia 4402 kufutia harambee iliyo kuwa imeandaliwa na Halmashauri hiyo ya kuchangia madawati kwa Shule za Msingi na Sekondari ili waweze kumaliaza tatizo hilo kufikia 30 june

Harambee hiyo iliyofanyikia katika ukumbi wa Halmashauri hiyo iliyoongozwa na Mkuu waWilaya hiyo Joshua Mirumbe  aliwataka Watendaji wa Vijiji na Kata kusimamia jambo hilo kwa umakini ili kutatua tatizo la wanafunzi kukaa chini wakati wakiwa darasani.

 Mirumbe aliwataka wadau wa Elimu mbalimbali  walio shiriki harambee hiyo wakiwamo Wafanyabiashara,wafugaji,Walimu wakuu wa Shule za msingi na Sekondari, Waratibu Elimu,Maafisa Tarafa ,Wakuu wa Idara ya halmashauri hiyo, Madiwani pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda kujitoa kwa Moyo katika zoezi hilo ili kusaidia kukuza Elimu ya Watoto wao.


"Kama Taifa hili hatutalisaidia katika Elimu tutalua" Alisema Mirumbe
                        Wadau wa Elimu wakiwa katika harakati za kutokomeza kero ya madawati
Mirumbe alisema pamoja na jitihada zilizo onyeshwa na Halmashauri hiyo za kupunguza tatizo hilo kutoka upungufu wa awali wa Madwati 14000 hadi  kufikia 4402 lakini bado inachangamoto ya kumaliza tatizo hilo haraka iwezekanavyo kabla ya mwisho wa agizo lililo tolewa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli.

Halmashuri hiyo inajumla ya shule za Msingi 101 huku jumla ya shule za sekondari zikiwa 7.


Awali akifungua harambee hiyo Mirumbe alisema "Kilio kinaanzwa na wenye kilio  hivyo basi ni lazime tulie sisi wenyewe kabla yakutafuta msaada kutoka nje"

 Ikumbukwe Rais Magufuli aliziagiza halmasshauri zote nchini kuhakikisha kwamba zinamaliza tatizo la madwati katika shule zote kabla ya Juni 30 mwaka huu vinginevyo hatasita kumwajibisha mkuu wa wilaya husika pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri husika. 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni