Jumamosi, 28 Mei 2016

JOSHUA MIRUMBE AWATAKA WAKAZI WA WILAYA YA BUNDA KUJITOKEZA SIKU YA TAREHE 31.05.2016 KATIKA HARAMBEE YA UCHANGIAJI MADAWATI.





Mkuu wa wilaya ya Bunda Joshua Chacha Mirumbe amewataka wakazi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi siku ya uchangiaji madawati inayotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo siku ya Jumanne saa nne asubuhi.

Mirumbea aliyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake ambapo aliseme ni wakati sasa wa wakazi wa Bunda kuonyesha uzalendo wao katika changamoto hii ambayo imekuwa kilio kila kona ya nchi ya Tanzania jambo ambalo linatajwa ni moja ya sababu ya wanafunzi kufeli mitihani yao.

“Ni wakati wa wakazi wa bunda kuchukua hatua madhubuti ya kuhakikisha watoto hawakai chini katika shule za sekondari na za msingi” aliseme Mirumbe.

Akihitimisha taarifa hiyo ya uchangiaji madawati kwa vyombo vya habari  Mirumbe alisema kwa Yule atakayeshindwa kufika siku hiyo ni vyema mchango wake akawasilisha kwa kiogozi yeyote aliyekaribu naye.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni