Jumamosi, 28 Mei 2016

Mkutano wa Trump wakabiliwa na ghasia



Polisi wa kukabiliana na ghasia nchini Marekani walitumwa kwenye mji wa San Diego, jimbo la California, kuzuia makabiliano kati ya maelfu ya wafuasi na wanaompinga mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump.

Waandamanji hao walipeperusha bendera za Marekani na Mexico, wakati bwana Trump akitoa hotuba yake.

San Diego, ni kilomita chache tu kutoka mpaka wa Mexico na Marekani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni