Mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Kilimanjaro imekamata bidhaa kutoka nje za mamilioni ya fedha baada ya kuvushwa kwa njia ya magendo katika maeneo ya Kitobo, Kileo na Njiapanda zikisafirishwa kwa njia ya magari mawili na pikipiki tano.
Meneja wa TRA wa mkoa huo Bw. Abdul Mapembe alisema kuwa,
katika oparesheni hiyo ya kudumu wameyakamata magari mawili moja likiwa
na usajili wa kenya likiwa na bidhaa hizo vikiwemo vifaa vya magari,
televisheni. Pikipiki, simu za mkononi, nguo, mafuta ya taa, chumvi na
sukari.
Bw.Mapembe alisema, wafanyabiashara wa bidhaa hizo baada ya
kukamatwa walitakiwa wakalete vielelezo vya bidhaa zao kama wamezilipia
ushuru mpakani kama walivyodai lakini hawajaonekana.
Kiongozi wa oparesheni hiyo Bw. Obednego Nicholaus amewaonya wenye
magari na pikipiki hizo kuwa kama hawatajitokeza kulipia ushuru bidhaa
zitataifishwa pamoja na magari hayo aina ya fuso na pikipiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni