Wizara ya mambo ya nje nchini India inasema imeitisha taarifa kutoka kwa maafisa wa jiji la Hyderabad baada ya mwanafunzi kutoka Nigeria kushambuliwa Jumatano.
Mwanafunzi huyo alitibiwa hospitalini na baadaye kuruhusiwa kuondoka.
Wiki iiyopita, kijana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alipigiwa na kuuawa mjini Delhi.
Kisa hicho kiliwafanya mabalozi wa nchi za Afrika kutishia kususia sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika nchini India ingawa baadaye walibadilisha msimamo wao.
Baada ya kuripotiwa kwa kisa hicho, maduka ya raia wa India katika mji mkuu wa Dr Congo, Kinshasa yalivamiwa na kuporwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni