Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameombwa na baadhi ya wananchi mkoani Kagera kutimiza ahadi yake aliyoitoa ya kununua meli mpya itayotumia Ziwa Victoria kutoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo kati ya bandari ya Bukoba na Mwanza ili waweze kuondokana na hadha ya usafiri wa majini wanayokumbana nayo kwa sasa baada ya meli za Mv. Serengeti na Mv. Victoria zilizokuwa zikitoa huduma hiyo kusimamishwa kutokana na ubovu uliokuwa ukihatarisha usalama wa mizigo na abiria.
Baadhi ya wananchi hao ambao hutegemea zaidi huduma usafiri wa
majini kusafirisha mizigo yao na kusafiri pi ambayo hutolewa na kampuni
ya Taifa ya huduma za meli, wakizungumza na ITV wakiwa kwenye eneo la
bandari ya Bukoba wamesema hatua ya kusimamishwa kwa huduma ya usafiri
wa meli kati ya bandari ya Bukoba na Mwanza kuwa imewaathiri sana kwa
kuwa kwa sasa mizigo yao mingi wanaisafirisha kwa kutumia njia ya
barabara jambo linalowagharimu fedha nyingi, wamesema meli za Mv.
Serengeti na Mv. Victoria hazifai kutoa huduma ya usafiri hata
zikifanyiwa matengenezo.
Kwa upande wake, Afisa wa kampuni ya Taifa ya huduma za meli katika
bandari ya Bukoba, Mathias Mathew akizungumza amesema meli ya Mv.
Serengeti itaanza kutoa huduma baada ya kufanyiwa ukarabati, amesema
meli ya Mv. Serengeti ambayo ni meli pekee iliyokuwa ikitoa huduma ya
usafiri kati ya bandari ya Mwanza na Bukoba ilisimamishwa kutoa huduma
ya usafiri Machi 21, mwaka huu kutokana na ubovu jambo ambalo limeitia
hasara kampuni hiyo zaidi ya shilingi zaidi ya milioni 432 kwa kuwa kila
juma ilikuwa ikiingiza zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni