BUNDA. habari na Gharos Riwa
Halmashauri
za vijiji zimetakiwa kuwa na ushirikiano wa karibu na ngazi za juu za kiserikali
ili kuharakisha maendeleo katika maeneo yao.
Wito huo
ulitolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa bunda mh, Pius Mayaya wakati
alipokuwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha nyasana katika kata ya kabasa
wilayani humo katika sherehe za uzinduzi wa ofisi mpya ya serikali ya kijiji
hicho kilicho gharimu shilingi milioni tisa laki sita na mia nne.
Alisema
kuwa ushirikiano huo unatasaidia
upatikanaji wa taarifa sahihi kwa viongozi wa ngazi za juu na kuchukua hatua za
haraka kutatua changamoto zinazojitokeza
na kuongeza kwa kutolea mfano nguzo za umeme zilizokuwa zinataka kuhamishwa
kutoka katika kijiji hicho na shirika la umeme tanesco wilayani bunda pasipo kushirikisha serikali ya kijiji jambo ambalo lililoshindikana mara baada ya taarifa
kufikishwa katika ngazi ya halmashauri ya mji.
Aidha Mayaya
aliwataka viongozi wa serikali ya kijiji hicho kuwasomea wananchi mapato na
matumizi kila baada ya miezi mitatu ili wananchi wafahamu mwenendo wa maendeleo
yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni