
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ramadhani Ng"hazi alisema kuwa Mwalimu Matiku anadaiwa kumuanganisha mwanafunzi wa kike aliye kuwa akisoma darasa la shuleni hapo na kijana aliyekuwa akimuuzia duka lake.
Alisema kutokana na Mapenzi hayo binti huyo mwenye umri wa miaka kumi na sita kalipata ujauzito wa miezi sita ulio gundulika mapema mwaka huu baada ya kupimwa akiwa katika shule moja ya sekondari anako soma kwa sasa
“Mwaka jana nikiwa darasa la saba mwalimu alinipeleka nyumbani kwake ili nikamsaidie kukamua ng’ombe maziwa, siku ya pili wakati wa mapumziko alinichukua nikamuoshee vyombo tulimkuta huyo kijana baadaye mwalimu alinisihi nibaki naye ndani,” alidai. .
Kamanda Ng"hazi alisema baada ya kuhojiwa binti huyo alimtaja kijana aliyempatia mimba na kwamba aliye muunganisha na kijana huyo ni mwalimu wake ambaye alikuwa akimtoadarasani mara kwa mara kumpeleka kwa huyo kijana
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni