Mwanamke mmoja nchini India amejifungua mtoto wa uzani wa kilo 6.8 ambaye madaktari wanasema huenda akawa mtoto mwenye uzani wa juu zaidi kuwahi kuzaliwa nchini humo.
Mtoto huyo ana uzani sawa na mtoto wa umri wa miezi sita.
Nchini humo, watoto huzaliwa na uzani wa kadiri wa kilo 2.5-3.5.
Mamake Nandini, 20, alijifungua kupitia upasuaji katika jimbo la Karnataka, kusini mwa nchi hiyo.
Afisa wa afya wa hospitali ya wilaya ya Hassan, Dkt Venkatesh R, ameambia BBC kwamba mtoto huyo pia ni mrefu wa kimo.
Mtoto huyo ana kimo cha sentimeta 62 (inchi 24.4in) ilhali kwa kawaida watoto India huzaliwa na kimo cha sentimeta 50,"amesema Dkt SR Kumar, anayemtunza Nandini na mwanawe.
Visa vya watoto kuzaliwa na uzani wa juu kupindukia sana hutokana na mama kuugua kisukari lakini madaktari wamebaini Nandini hana tatizo hilo.
Rekodi ya mtoto mwenye uzani wa juu zaidi India inashikiliwa na mvulana aliyezaliwa na Firdous Khatun jimbo la Uttar Pradesh Novemba 2015. Mvulana huyo alikuwa na uzani wa kilo 6.7.
Rekodi ya dunia inashikiliwa na mvulana aiyezaliwa na Carmelina Fedele eneo la Aversa, Italia, mwezi Septemba 1955. Alikuwa na uzani wa kilo 10.2.
mjulishe na nduguyo au jamaa kadri uwezavyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni