Ijumaa, 27 Mei 2016

MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WA TILIA MKAZO SEKTA YA KILMO

BUNDA :Na mwandishi Christopher Maregesi
Baadhi ya Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Bunda Mkoani Mara wameitaka idara ya kilimo ya halmashauri hiyo kuwachukulia hatua za kisheria mawakala wa pembejeo ambao wamekuwa wakifanya kazi zao kwa kubabaisha.
Wakiongea kwenye kikao cha baraza la halmashauri hiyo madiwani hao wamesema baadhi ya mawakala hao wamekuwa wakitoa taarifa za utendaji kazi wao tofauti na hali halisi ilivyo  jambo linalo changia kuzorota kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo wilayani humo.
Mmoja wa madiwani hao mramba Simba Nyamkinda wa kata ya ketare amesema katika kudhibiti hali hiyo halmashauri haina budi kuweka mfumo maalumu wa kufuatilia nyendo za mawakala hao ili wale watakao bainika kuwa wababaishaji waadhibiwe kisheria.
Hata hivyo afisa kilimo wa halmashauri hiyo Serapion Rujuguru licha ya kukiri kuwepo kwa mawakala wasio waaminifu ambao halmashauri imewaadhibu kisheria lakini pia amewataka madiwani kusaidia kuwadhibiti mawakala hao.








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni