Jumanne, 31 Mei 2016

MADIWANI WASEMA MAWAKALA WABABAISHAJI WACHUKULIWE HATUA





 Baadhi ya Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Bunda Mkoani Mara waliitaka idara ya kilimo ya halmashauri hiyo kuwachukulia hatua za kisheria mawakala wa pembejeo ambao wamekuwa wakifanya kazi zao kwa kubabaisha.
Wakiongea kwenye kikao cha baraza la halmashauri hiyo madiwani hao walisema baadhi ya mawakala hao wamekuwa wakitoa taarifa za utendaji kazi wao tofauti na hali halisi ilivyo  jambo linalo changia kuzorota kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo wilayani humo.
Mmoja wa madiwani hao mramba Simba Nyamkinda wa kata ya ketare alisema katika kudhibiti hali hiyo halmashauri haina budi kuweka mfumo maalumu wa kufuatilia nyendo za mawakala hao ili wale watakao bainika kuwa wababaishaji waadhibiwe kisheria.
Hata hivyo afisa kilimo wa halmashauri hiyo Serapion Rujuguru licha ya kukili  kuwepo kwa mawakala wasio waaminifu ambao halmashauri imewaadhibu kisheria lakini pia aliwataka madiwani kusaidia kuwadhibiti mawakala hao

JKT YATOA NYONGEZA YA MAJINA YA VIJANA WA KIDATO CHA SITA KABLA YA TAREHE 10 MWEZI WA 6

 
Vijana wafuatao wameongezwa kuhudhuria mafunzo ya jkt katika makambi mbalimbali kama inavyoonekana hapo chini.

Pia baadhi ya vijana wamehamishwa makambi kutokana na sababu mbalimbali.Waripoti kwenye makambi kama inavyoonekana  hapa chini kabla ya tarehe 10 juni 2016.

S/NO    JINA                                                        KIKOSI
1     ABDILLAH RAMADHANI HAJI         MGAMBO JKT
2     ABDUL M. MTEKETA         MGAMBO JKT
3     ABDULAZIZ SALUM AHMAD         MARAMBA JKT
4     AGNES PETER MAGANGA         RUVU JKT
5     AGNESS EMMANUEL KITANDU         RUVU JKT
6     AGNESS PETER MAGANGA         MARAMBA JKT
7     AJUAE DAVIS AMINIELI         KANEMBWA JKT
8     ALEX MLOSO         MARAMBA JKT
9     ALFRED AIDAN MBANO         RUVU JKT
10     ALLY KAFERA ALLY         KANEMBWA JKT
11     ALVIN ISMAEL MAKUNDI         RUVU JKT
12     AMBWENE FRANK MWAKANEMA         MARAMBA JKT
13     AMOS ASEGE         RUVU JKT
14     AMOS KINGU         MARAMBA JKT
15     ANNA JORAM TIMBA         RUVU JKT
16     ANNA M. JANUARY         MSANGE JKT
17     ANTIA PANCRAS KAKWERA         RUVU JKT
18     AVITUS MUSHABI         RUVU JKT
19     BEATRICE BONFACE         MARAMBA JKT
20     BEAUTNESS JOHN NJAU         RUVU JKT
21     BENJAMIN STEPHEN NYANDA         RUVU JKT
22     BERNADINAH T. MAYOMBYA         RUVU JKT
23     BIBIANA CLETUS NJOKHA         RUVU JKT
24     BONIFACE DEOGRATIUS         RUVU JKT
25     BONIFACE JOHN         RUVU JKT
26     BRENDA JOHN BABU         MARAMBA JKT
27     BUNURI JUMA         RUVU JKT
28     CALISTER MKOLO         RUVU JKT
29     CAROLINE HENRY KABOGO         MARAMBA JKT
30     CAROLINE SOSTHENES MAHERI         RUVU JKT
31     CECILIA MPEMBA         RUVU JKT
32     CLEMENCE GWINO         RUVU JKT
33     COSTANTINE PETER         RUVU JKT
34     DANIEL BENEDICT MASHIKU         MAKUTOPORA JKT
35     DAVID L. MARIBA         RUVU JKT
36     DAVID R. MKUMBO         RUVU JKT
37     DENIS G SADALA         MARAMBA JKT
38     DEOUS SILIVESTA LUBINGA         RUVU JKT
39     DIALO MNYUKI         MAFINGA JKT
40     DICKSON JOCTAN MATOGO         MARAMBA JKT
41     DONAT ERENEST MAJALA         MAKUTOPORA JKT
42     DONATH ERNEST MAJALA         MAKUTOPORA JKT
43     DORCUS DEOGRATIUS         RUVU JKT
44     EDDAH SAUL ASWILE         RUVU JKT
45     EDWARD MMBARA MKIZU         MARAMBA JKT
46     ELAIN DIDAS MUTABINGWA         RUVU JKT
47     ELIAN E. NGONDO         RUVU JKT
48     ELINAZI YOAZ MSUYA         RUVU JKT
49     ELIZABETH DANIEL KIYABO         MGAMBO JKT
50     ELIZABETH MWAKITEGA         RUVU JKT
51     ELVIS MAHENGE SIMON         RUVU JKT
52     EMMA A. KILONZO         RUVU JKT
53     EMMANUEL PHILIPO         MGAMBO JKT
54     EVELYNE SCARION         RUVU JKT
55     EZEKIEL KWAKA MSESE         RUVU JKT
56     FABE MAGNUS NGONYANI         MAKUTOPORA JKT
57     FANUEL VICTOR KISIRI         RUVU JKT
58     FELICIAN PASCHAL ULAYA         RUVU JKT
59     FESTO MWAKAYO         RUVU JKT
60     FRANCES MASHAKA LUJAJI         RUVU JKT
61     FRODIANUS FIDERI         RUVU JKT
62     GABRIEL PATRICK LWESYA         MLALE JKT
63     GAUDENSIA MOHAMED MWALUNGWE         MAKUTOPORA JKT
64     GEORGE STANSLAUS SHAYO         RUVU JKT
65     GEORGIA ISHENGOMA         RUVU JKT
66     GERVAS PASCHAL KIHANGA         RUVU JKT
67     GETRUDE J. MASIMBANI         RUVU JKT
68     GIFTI A. LUGOME         MARAMBA JKT
69     GLORIA ALBERT MARINGO         RUVU JKT
70     GODFREY CHRISTIAN ROEBERT         RUVU JKT
71     GOODLUCK JOHN WILLSON         MGAMBO JKT
72     GREEN EUSTAD         RUVU JKT
73     GROLIA GODWIN KAHWA         MAFINGA JKT
74     HAJI SHEMHILU         RUVU JKT
75     HAPPINESS MGURU         RUVU JKT
76     HARRISON DAVID MRANGO         RUVU JKT
77     HASSAN RAJABU NJAU         RUVU JKT
78     HAWA ISSA MDENG'O         MARAMBA JKT
79     HAWA ISSA MDENG'O         MARAMBA JKT
80     HERI MOHAMED MKUMBEGE         RUVU JKT
81     HERIETH MAHENGE         RUVU JKT
82     HINDU HAMIS MRISHO         RUVU JKT
83     IBRAHIM ABDALLAH         RUVU JKT
84     IELEEN DIDAS MUTABINGWA         RUVU JKT
85     IMELDA IGNAS MBUNDA         MAKUTOPORA JKT
86     INZARI CHARLES LUGUTU         BULOMBORA JKT
87     IRENE KYENKUNGU         RUVU JKT
88     JACKLINE ADAM LEYNA         MGAMBO JKT
89     JACKLINE HERBET STEWARTH         MARAMBA JKT
90     JACKSON LUPAKISYO MWAIPUNGU         RUVU JKT
91     JAFARI S. JAFARI         RUVU JKT
92     JANE MGINJA MTIMBA         RUVU JKT
93     JANETH FORTUNATUS WAMBURA         RUVU JKT
94     JANETH V. KILONZO         RUVU JKT
95     JAPHET MASOTA         MARAMBA JKT
96     JASMIN MARTIN         RUVU JKT
97     JASMIN MARTIN SHAYO         MARAMBA JKT
98     JASMINE RASULI         RUVU JKT
99     JASON STEVEN         RUVU JKT
100     JIDIRU IZADINI KALOKOLA         RUVU JKT
101     JOHANITHA JOHN         MAFINGA JKT
102     JOHNSON JONATHAN JOHN         RUVU JKT
103     JORAM MBOMA JONATHAN         RUVU JKT
104     JOSEPH E. JOHNSON         MARAMBA JKT
105     JOSEPH REGNALD TUNGALAZA         RUVU JKT
106     JOSEPH TARIMO         RUVU JKT
107     JOSEPHINE BONIFACE MHANDO         RUVU JKT
108     JUENI MALIJANI         RUVU JKT
109     JUSTINE REGNALD MAKENE         RUVU JKT
110     KELVIN GEDION LEMNGE         MARAMBA JKT
111     KHADIJA E. KALONGA         RUVU JKT
112     KIBIBI HASAN JAMBIA         MARAMBA JKT
113     LAULENCIA ENGITRAUDA         842KJ
114     LEAH THOMAS MTWEVE         RUVU JKT
115     LILAN HENRY CASTORY         MAKUTOPORA JKT
116     LILIAN KANG'WA MASANJA         RUVU JKT
117     LUCIA JORAM TIMBA         RUVU JKT
118     LUGENDO LUCAS CHAPUGA         RUVU JKT
119     MARIAM M. JUMA         RUVU JKT
120     MARIAM WAMBURA         MSANGE JKT
121     MARIAMU S LIPENDE         MAKUTOPORA JKT
122     MARKO MICHAEL KASONI         RUVU JKT
123     MARTIN EWALD MALYAWERE         RUVU JKT
124     MARTINA GEORGE MWAILUSI         RUVU JKT
125     MARY ANTHONY MASSAWE         RUVU JKT
126     MARY I MREMA         MAKUTOPORA JKT
127     MASTERBETTER JOHN         RUVU JKT
128     MATHIAS BAHATI ORESTI         MAKUTOPORA JKT
129     MESHACK MARTIN LYIMU         MARAMBA JKT
130     MESHACK MARTIN LYIMU         RUVU JKT
131     MICHAEL DEOGRATIUS NJAU         MGAMBO JKT
132     MIRIAM M. JUMA         RUVU JKT
133     MUSSA KALUME AGUSTINE         RWAMKOMA JKT
134     MUSSA S. MAIGE         RUVU JKT
135     MWAMINI KADUMA         RUVU JKT
136     NAISHOOKI WILBERT OLE-MBILE         RUVU JKT
137     NAOMI ENMANUEL LEKASHINGO         MARAMBA JKT
138     NASRA NURDIN YUSSUPH         RUVU JKT
139     NEEMA JAMES MANYAMA         RUVU JKT
140     NEEMA MAIKO MASAGASI         RUVU JKT
141     NEEMA MSUYA         RUVU JKT
142     NESTARY AGATHON NDUNGURU         MAFINGA JKT
143     NESTARY AGATON NDUNGURU         MAFINGA JKT
144     NICODEMO JACOB         RUVU JKT
145     NOEL JAMES MWAKISOMBE         RUVU JKT
146     NORBERT NOEL         KANEMBWA JKT
147     NUSRAT ZAKARIA         RUVU JKT
148     OCTAVIAN BUBERWA         RUVU JKT
149     OMARI DIWANI OMARI         RUVU JKT
150     OMARY MAKOTA ALLY         KANEMBWA JKT
151     PAUL KATUNZI         MSANGE JKT
152     PRISCILA WENDE MGANA         MAKUTOPORA JKT
153     PROJESTUS H.CHAMAHANGA         RUVU JKT
154     RACHEL DAVID ISSAME         RUVU JKT
155     RACHEL DAVID ISSAME         RUVU JKT
156     RACHEL RAYMOS FOYA         RUVU JKT
157     RAHEL FESTUS ISOKOZA         RUVU JKT
158     RAMADHANI ALLY NJERA         RUVU JKT
159     RAMADHANI MBWAMBO         MARAMBA JKT
160     RAMADHANI RAJABU RAMADHANI         RUVU JKT
161     RAMADHANI RAJABU RAMADHANI         RUVU JKT
162     RECHO DANIEL MWALIMU         MAKUTOPORA JKT
163     REHEMA DEUS RUBALE         RUVU JKT
164     REHEMA SHAWARI IKAJI         MARAMBA JKT
165     REMIDIUS REYMOND MUTA         RUVU JKT
166     RETISIA SAANANE         RUVU JKT
167     RIDHIWANI SHABANI MAKUMBI         MGAMBO JKT
168     RISHAD KIHOMO MLELWA         RUVU JKT
169     ROGERS JOHN EZEKIEL         RUVU JKT
170     ROMAN CASTORY         RUVU JKT
171     ROSEMARY T. MASIAGA         MSANGE JKT
172     SADICK HASHIM MWAISAKA         RUVU JKT
173     SAIMON P. SOZIGWA         MARAMBA JKT
174     SALA A. MWAKAJWANGA         RUVU JKT
175     SALEHE MACHIBYA JONIOR         MGAMBO JKT
176     SALMIN AMRI         MARAMBA JKT
177     SALOME AMOS         RUVU JKT
178     SALOME SHITUNGURU         RUVU JKT
179     SHUKRANI MWAIPWISI         MAFINGA JKT
180     SIMON P. SOZIGWA         RUVU JKT
181     SOLINA SABAS         RUVU JKT
182     SOPHIA DEUS RUBALE         RUVU JKT
183     SOPHIA S. MATHIAS         MARAMBA JKT
184     STEPHEN F. NDALUSE         RUVU JKT
185     STIVEN NDALUSO         RUVU JKT
186     SUSAN PATRICK MNASIZU         RUVU JKT
187     SWEED IDD         RUVU JKT
188     TATU HAMAD HATIBU         RUVU JKT
189     TATU JUMA MYOVELA         MARAMBA JKT
190     TOMESTECLES H.CHAMAHANGA         RUVU JKT
191     TUMAINI JOHN MAKUNENGE         BULOMBORA JKT
192     TUMPALE JAPHET         RUVU JKT
193     VAILET GEORGE SIMBA         RUVU JKT
194     VALERIAN VEREMUND CHARLE         MAFINGA JKT
195     VERONICA CASMIR NDAMBARIKA         MAKUTOPORA JKT
196     VERUS THOBIAS KASONSO         RUVU JKT
197     VERUS TOBIAS KASONSO         RUVU JKT
198     VICTOR DAUDI ANYASIME         RUVU JKT
199     VICTOR L. AMBELE         RUVU JKT
200     VICTORY HENRY         RUVU JKT
201     WALTER FRUGENCE SAMKY         RUVU JKT
202     WILLIAM OSIAS MWANYIKA         RUVU JKT
203     WILLIAM PATRICK ASSEY         MGAMBO JKT
204     YASSER HAMAD MALESA         MARAMBA JKT
205     ZAMDA MWALIMU         MAKUTOPORA JKT

MWALIMU ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUMUUNGANISHA MWANAFUNZI KIMAPENZI.


Jeshi la Polisi mkoani Mara linamshilia mwalimu wa shule ya msingi Nyigabo iliyopo kijiji cha Musati  wilayani Serengeti ambaye ni Agnes Matiku kwa kosa la kumfanyia mpango wa kimapenzi kijana mwanafunzi wa shule hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ramadhani Ng"hazi alisema kuwa Mwalimu Matiku anadaiwa kumuanganisha mwanafunzi wa kike aliye kuwa akisoma darasa la shuleni hapo na kijana aliyekuwa akimuuzia duka lake.

Alisema kutokana na Mapenzi hayo  binti huyo mwenye umri wa miaka kumi na sita kalipata ujauzito wa miezi sita ulio gundulika mapema mwaka huu baada ya kupimwa akiwa katika shule moja ya sekondari anako soma kwa sasa 


 “Mwaka jana nikiwa darasa la saba mwalimu alinipeleka nyumbani kwake ili nikamsaidie kukamua ng’ombe maziwa, siku ya pili wakati wa mapumziko alinichukua nikamuoshee vyombo tulimkuta huyo kijana baadaye mwalimu alinisihi nibaki naye ndani,” alidai. .

Kamanda Ng"hazi alisema baada ya kuhojiwa binti huyo alimtaja kijana aliyempatia mimba na kwamba aliye muunganisha na kijana huyo ni mwalimu wake ambaye alikuwa akimtoadarasani mara kwa mara  kumpeleka kwa huyo kijana















































MIRUMBE AFANIKISHA KUCHANGISHA JUMLA YA MADAWATI 326 KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA.

Halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara imefanikiwa kupunguza upungufu wa madawati kutoka 4728 hadi kufikia 4402 kufutia harambee iliyo kuwa imeandaliwa na Halmashauri hiyo ya kuchangia madawati kwa Shule za Msingi na Sekondari ili waweze kumaliaza tatizo hilo kufikia 30 june

Harambee hiyo iliyofanyikia katika ukumbi wa Halmashauri hiyo iliyoongozwa na Mkuu waWilaya hiyo Joshua Mirumbe  aliwataka Watendaji wa Vijiji na Kata kusimamia jambo hilo kwa umakini ili kutatua tatizo la wanafunzi kukaa chini wakati wakiwa darasani.

 Mirumbe aliwataka wadau wa Elimu mbalimbali  walio shiriki harambee hiyo wakiwamo Wafanyabiashara,wafugaji,Walimu wakuu wa Shule za msingi na Sekondari, Waratibu Elimu,Maafisa Tarafa ,Wakuu wa Idara ya halmashauri hiyo, Madiwani pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda kujitoa kwa Moyo katika zoezi hilo ili kusaidia kukuza Elimu ya Watoto wao.


"Kama Taifa hili hatutalisaidia katika Elimu tutalua" Alisema Mirumbe
                        Wadau wa Elimu wakiwa katika harakati za kutokomeza kero ya madawati
Mirumbe alisema pamoja na jitihada zilizo onyeshwa na Halmashauri hiyo za kupunguza tatizo hilo kutoka upungufu wa awali wa Madwati 14000 hadi  kufikia 4402 lakini bado inachangamoto ya kumaliza tatizo hilo haraka iwezekanavyo kabla ya mwisho wa agizo lililo tolewa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli.

Halmashuri hiyo inajumla ya shule za Msingi 101 huku jumla ya shule za sekondari zikiwa 7.


Awali akifungua harambee hiyo Mirumbe alisema "Kilio kinaanzwa na wenye kilio  hivyo basi ni lazime tulie sisi wenyewe kabla yakutafuta msaada kutoka nje"

 Ikumbukwe Rais Magufuli aliziagiza halmasshauri zote nchini kuhakikisha kwamba zinamaliza tatizo la madwati katika shule zote kabla ya Juni 30 mwaka huu vinginevyo hatasita kumwajibisha mkuu wa wilaya husika pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri husika. 
 

Jumatatu, 30 Mei 2016

Wakulima wahimizwa kuzalisha pamba safi na yenye kiwango





WAKULIMA na wanunuzi wa zao la pamba, katika mikoa ya kanda ya Mangaribi, wamehimizwa kuzingatia ubora wa zao na usafi wa zao hilo, ili liweze kupata soko la uhakika.

Rai hiyo ilitolewa juzi katika Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, na mkaguzi wa viwanda vya pamba mwandamizi, Kisinza Ndimu, kwenye semina ya ubora na usafi wa pamba, kwa wanunuzi wa pamba mbegu ngazi ya vituo, iliyofanyika katika ukumbi wa kiwanda cha kampuni ya Oram LTD mijini Bunda.

Ndimu alisema wakulima na wanunuzi wa zao hilo wamekuwa wakiharibu kwa makusudi ubora na usafi wa zao la pamba, hali ambayo imekuwa ikisababisha thamani yake kushuka kila mwaka.
Alisema wanunuzi wamekuwa wakifanya uharibifu huo kwa asilimia zaidi ya 80 wakati inapofika katika vituo vyao vya kununulia pamba na akayataka makundi yote mawili, pamoja na wadau mbalimbali kuzingatia ubora na usafi wa zao hilo.

“Watu wamekuwa wakiharibu kwa makusudi kabisa ubora na usafi wa zao la pamba, wanaweka maji, mchanga na vitu vingine ambavyo havifai kabisa ili kushusha ubora, ” alisema Ndimu.
Ofisa mwandamizi wa zao la pamba nchini, Emily Mbagulle, alisema ni jukumu la kila mdau wa zao la pamba, kuzingatia ubora wa zao hilo, kuanzia wakati wa kuandaa shamba, kulima, kuvuna, kuhifadhi, pamoja na wakati wa kuuza ili kuimarisha uboa wake.
“Hili ni jukumu letu sote kuhakikisha tunalinda na kuimaraisha ubora wa zao la pamba maana wote tunalitegemea zao hili,” alisema.

Akichangia hoja katika semina hiyo Meneja wa kiwanda cha Oram Tanzania LTD, Dick Chiriwo, kilichoko wilayani Bunda, aliwahasa wanunuzi wa zao hilo, kujenga mshikamano wa pamoja kwa kuacha kununua pamba ambayo haina ubora, kwa lengo la kupata pamba nyingi maana hiyo itakuwa ni hasara kwao.

“Wote wanunuzi mkishakamana na kukataa kabisa kununua pamba chafu mtakomesha hali hii….sasa unakuta mwingine anakataa kununua pamba chafu lakini mwingine wa sehemu hiyo hiyo anaikimbilia eti aweze kupata pamba nyingi, hiyo ni hasara kwenu acheni kabisa na wote mshikamane,” alisema Chiriwo.
Baadhi ya wanunuzi wa zao hilo wakiwemo wakulima na wanunuzi walisema kuwa kuna changamoto nyingi zinazowakabili wakulima, ikiwa ni pamoja na ya kutokupata pembejeo kwa wakati, pamoja na kupewa dawa za kuua wadudu ambazo hazina uwezo, pamoja na mbegu ambazo hazioti.

Jumapili, 29 Mei 2016

Jamii imetakiwa kuachana na imani za kishirikina




Jamii imetakiwa kuachana na imani za kishirikina zinazopelekea uvunjifu wa amani na badala yake waelekeze imani yao kwa mwenyezi mungu hali itakayo wawezesha kuishi kwa amani na upendo.

Hayo yamesemwa na Askofu mkuu wa kanisa la methodist kanda ya afrika mashariki na kati Joseph Ntombura kupitia mafundisho yake aliyoyatoa kwenye mkutano maalum wa injili uliofanyikia mjini Bunda.

Askofu Ntombura amesema kama jamii itamwelekea Mungu  vitendo viovu kama vile rushwa na ubadhirifu uliokithiri vitatoweka na hivyo wengi wao kufanya mambo yenye tija kwa makuzi ya uchumi wa taifa.

Aidha  Askofu Ntombura ametumia  furusa hiyo kuendesha huduma maalum ya kumuombea Rais Dkt.John Pombe Magufuli ili azidishiwe busara na hekima katika utendaji kazi wake wa kuliongoza vema taifa la Tanzania.







Wanafunzi 7,000 watemwa UDOM





Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimewasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada na kuwataka waondoke chuoni hapo mara moja.

Jana, lilitolewa tangazo chuoni hapo likiwataka wanafunzi hao kuondoka kati ya jana hadi leo saa 12 jioni. Tangazo hilo lilieleza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo katika ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao kurejea majumbani na wataelezwa mustakabali wao “mapema iwezekanavyo”.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alipotakiwa kufafanua suala hilo, alisema kwa ufupi kuwa suala hilo lipo lakini akaelekeza apigiwe simu Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Beatrice Baltazal kwa maelezo zaidi.

Baltazal alipotafutwa alisema kusimamishwa kwa wanafunzi hao kulitokana na agizo la Serikali na wametakiwa kulitekeleza.

Kuhusu lini na nini hatima ya wanafunzi hao, alisema bado hawajui hadi hapo watakapoelekezwa vinginevyo.

Hata hivyo, kulikuwa na malalamiko kwa wanafunzi hao juu ya namna walivyopewa taarifa za kusimamishwa masomo yao kwa ghafla na kutakiwa kuondoka.

Kozi ya stashahada ya ualimu wa sayansi, ilianzishwa maalumu kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la walimu wa sayansi na ilikuwa inatolewa UDOM pekee.

Waliokuwa na sifa za kujiunga na kupewa mikopo ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kufaulu vizuri masomo ya sayansi. 

Wanafunzi hao waliokuwa wamekopeshwa na Serikali wamesimamishwa siku mbili baada ya wenzao zaidi ya 480 wa Chuo Kikuu cha St. Joseph kusimamishwa baada ya kubainika hawakuwa na sifa za kudahiliwa.