Jumanne, 5 Julai 2016

Watumishi wilayani Bunda watakiwa kufanya kazi kwa kusoma majira na nyakati.


Mkuu wa  wilaya ya Bunda Lidya Simeon Bhupilipili amewataka watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda na halmashauri ya mji  kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma na kusoma majira na nyakati katika utendaji wao wa kazi
Hayo aliyasema wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo katika ukumbi wa halmashauri ya bunda baada ya kufanya makabidhiano na aliye kuwa mkuu wa wilaya hiyo Joshua Chacha Mirumbe.
Fanyeni kazi kwa kujituma na kusoma majira na nyakati katika utendaji wenu wa kazi
Bhupilipili alisema kuwa watumishi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa kujiamini  bila kuwa na woga wala hofu kwa kufuata na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi CCM.
Kwa sasa tunaendesha serikali kwa kufuata ilani ya ccm na si vinginevyo
Aidha aliwaomba watumishi kuwa na  ushirikiano katika utendaji kazi wao ili waweze kuleta maendeleo katika wilaya ya Bunda na Taifa kwa ujumla huku akiwaonya  watumishi kuacha  utumiaji mbaya wa fedha na uandaaji wa  taarifa zisizo za kweli katika miradi  mbalimbali ya maendeleo kwa Wananchi.
Ni wambie tu kwa wale wapenda kuchakachua taarifa na utumiaji wa fedha vibaya niwape onyo tu kuwa acheni tabia hiyo
Awali mkuu wa wilaya mstaafu  Joshua cha cha Mirumbe aliwaomba watumishi wa halmashauri zote mbili kuonesha ushirikiano wa dhati kwa mkuu wa wilaya mpya   Bhupilipili katika kuleta maendeleo ya wananchi.
Ni waombe watumishi mshirikiane vizuri na mkuu huyu wa wilaya katika mambo ya maendeleo ya wananchi na kwa taifa kwa ujumla























Hakuna maoni:

Chapisha Maoni