Jumanne, 19 Julai 2016

Wananchi wa Bunda kufaidika na zao la mpunga



Kampuni ya Mak Grup lenye makao yake makuu Mjini Dodoma limekuja na mpango wa kuwasaidia wakulima wa zao la Mpunga wilayani Bunda mkoani Mara kupitia mradi wake mpya wa Mivos.

Akizungumza na wandishi wa habari Daudi Musa ambaye ni mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kama  mtoa huduma katika wilaya ya bunda alisema wakulima wengi wa zao hilo bado wanafanya kilimo cha zamani cha kutupa mipunga badala ya kuwa na kitalu cha kuotesha kisha kuhamisha mashambani.

“Lengo letu ni kuleta mbinu mpya au ya kisasa kwa wakulima wazao la mpunga ili kuhakikisha wanaachana na kilimo kilichopitwa na wakati” alisema Daudi

Alisema Mradi huo unafanyika chini ya Ofisi ya waziri mkuu na unatekelezwa kupitia halmashauri ya wilaya ikiwana lengo la kusaidia wakulima wa mpunga kuongeza uzalishaji,kuongeza thamani ya mazao yao pamoja na  kupata masoko.

“Tunahitaji wakulima wawe na uhakika wa kupata soko la kuuza mazao yao ili wanufaike nayo” alisema Daudi

Daud Alisema kupitia mradi huo wa Mivos  mafunzo mbalimbali  yatakayotolewa ili wakulima wajue namna bora ya kulima zao la mpunga na kuwaunganisha katika masoko.
Hata hivyo mradi huo utaanza katika  Kata nne za wilaya ya bunda zinazolima zao hilo huku akiongeza kuwa kupitia mradi huo wakulima wataweza kunufaika na mafunzo, namna ya kupata pembe jeo na masoko ya uhakika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni