Kilio cha wachinja nyama katika machinjio ya Bunda mjini
mkoni Mara cha kuboreshewa Mazingira ya machinjio yao sasa kimeisha baada ya
serikali ya halmashari hiyo kuelekeza nguvu kubwa ya kuboresha machinjio
hayo ili kuhakikisha nyama zinachinjwa
katika Mazingira mazuri.
WaChachinja
nyama hao walisema hatua iliyochukuliwa na serikali ya halmashauri yao ni nzuri
maana miundombinu muhimu haikuwepo katika eneo hilo hali ilikuwaikitishia usalama wa afya zao.
Amon John ni
mmoja wa wachinja nyama katika machinjio hayo alisema kuwa mwanzoni huduma muhimu kama vile maji na choo havikuwepo
na kwamba damu zilikuwa zinatiririka hovyo na hivyo kuchafua Mazingira ya
machinjio hayo huku watumiaji wakijisaidia miji jirani.
Pamoja hayo waliishukuru
halmashauri ya mji wa Bunda kwa kuonyesha nia ya kuwasaidia kutoka hatua waliyokuwa
kuwa hadi hatua nyingine jambo ambalo linawatia hamasa sasa ya kufanya kazi kwa
moyo mmoja.
“Kiukweli
tunaishukuri halmashauri yetu ya mji wa Bunda kwa kutujali na sisi wachinja
nyama maana tulikuwa tumesahaulika” walisema
Naye diwani
wa kata hiyo Joash kunaga alisema kuwa yeye kama kiongozi wa eneo hilo ataendelea
kuwasaidia wananchi wake kupitia michango yake katika vikao vya madiwani vya halmashauri
hiyo.
“Mimi
kama kiongozi wao nitahakikisha naendelea kuwapigania wananchi wangu kwa mambo
mazuri kupitia vikao tunavyokaa” alisema Joash
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni