Baraza la vijana wa chama cha Demkrasia na maendeleo
Chadema, [BAVICHA] Mkoani Mara limesema kuwa limewaandikisha vijana zaidi ya
300, kuunga mkono tamko la makam mwenyekiti Bavicha Taifa bwana Patrick Sosopi alilolitoa
mnamo 2.julai mwaka huu la kukutana Dodoma kwa kile walichokidai kuwa ni
kuisaidia jeshi la polisi dhidi ya chama cha mapinduzi CCM kutii sheria bila shuriti.
Katibu wa Bavicha mkoa wa Mara bwana Yohana
Kaunya wakati akizungumza na wandishi wa habari kuwa kufuatia kikao cha hivi karibuni
kilichofanyika wilayani Butiama Mkoani Humo, kilichohudhuriwa na Mwenyekiti wa
vijana Taifa Patrobas Katambi, katibu mkuu wa vijana Tifa Julias Mwita na
Edward Sembei Mwenezi wa vijana taifa alisema idadi hiyo ndiyo ya vijana waliojiandikisha kwajili ya kuelekea Dodoma.
"idadi hiyo ndiyo ya vijana waliojiandikisha kwajili ya kuelekea Dodoma kiukweli vijana wameitikia katika suala hili" alisema kaunya
Katibu huyo alidai kuwa Chama hicho kimeamua
kuchuakua hatua hiyo kwa kuzingatia
uwepo wa upungufu wa jeshi la polisi nchini, pamoja na kusimamia usawa wa
Kiemokrasia.
Alipoulizwa kuwa maamuzi hayo hawaoni kama ni
kuingilia majukumu ya jeshi la polisi katika majukumu yao na kuchochea vurugu
nchini Bwana Kaunya Alisema kuwa wanatambua
uchache wa jeshi la polisi na kuhakikisha haki katika Demokrasia inafuatwa.
"Niseme tu kuwa tunatambua uchache wa jeshi la polisi lakini sisi tunataka kuhakikisha haki katika Demokrasia inafuatwa" alisema kaunya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni