Wakati
kukiwa na ulinzi mkali mjini Dodoma kuelekea Mkutano Mkuu Maalumu wa
CCM, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limehamishia mkutano wake wa
kamati ya utendaji jijini Dar es Salaam.
Jana,
sekretareti ya CCM ilianza maandalizi kusafisha njia kwa ajili ya kikao
cha Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na baadaye Mkutano Mkuu uliopangwa
kufanyika Jumamosi.
Awali,
Bavicha ilikuwa imehamasisha vijana wa chama hicho kuja kwa wingi mjini
hapa kwa ajili ya “kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuzuia
mikutano ya kisiasa”, lakini Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
alifuta mpango huo akisema: “Waache wafu wawazike wafu wao”.
Pamoja
na Mbowe kuzuia, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi alisema wiki
iliyopita kuwa wameandaa mkutano wa Kamati ya Utendaji wa Baraza hilo
leo mjini Dodoma na ungefunguliwa na Mbowe.
Huku ulinzi ukizidi kuimarishwa, jana kulikuwa na uamuzi tofauti.
Mwenyekiti
wa Bavicha Mkoa wa Dodoma, Malambaya Manyanya jana alisema wameamua
kuuhamishia mkutano huo Dar es Salaam baada ya kuona mzozo umekuwa
mkali.
"Tumeona mzozo ni mkali sana. Tumeona imeshakuwa shida, tukaona ngoja tukafanyie Dar,” alisema Manyanya.
Alisema wajumbe waliokuwa waingie Dodoma jana, wameambiwa wote waelekee Dar es Salaam kwenye jengo la makao makuu
Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka yeye anasema
kutakuwa ulinzi mkali na hakuna atakayeweza kujaribu kuvuruga mkutano
huo ambao utashuhudia Rais John Magufuli akichaguliwa kuwa mwenyekiti
mpya wa chama hicho.
Ole
Sendeka alisema kwenye ukumbi mpya wa CCM ambako ndiko mkutano huo
utakafanyika, kutakuwa na kamera maalumu zitakazofungwa ndani na nje ya
ukumbi ili kuwezesha kuona kila kitu kinachoendelea.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama wa mkoa, alisema ameona kwenye mitandao ya kijamii
kwamba baadhi ya vyama vinatoa vitisho na kuwataka wananchi wavipuuze.
“Na
kama kuna mtu anadhani kuwa anaweza kukwamisha mkutano mkuu wa CCM,
nimwambie Dodoma si salama kwake. Afikirie mahali pengine, lakini si
Dodoma,” alisema.
“Nitumie
fursa hii kuwaomba wananchi pale wanapoona mtu wasiyemwelewa au dalili
waripoti haraka kwenye vyombo vya habari na dola au kwa viongozi popote
pale ambapo wanaweza kushirikiana kuliondoa hilo tatizo. Lakini kwa
ujumla hali iko shwari mpaka sasa,” alisema Rugimbana.
Wakati
Rugimbana akisema hayo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Mayalla
Towo amesema wameweka miundombinu ya kuweza kuwabaini wahalifu, lakini
hawezi kuitaja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni