Mwenyekiti
wa chama hicho, James Mbatia aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa
uamuzi huo umepitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.
Mbunge
huyo wa Vunjo na mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema makosa mengine
aliyokutwa nayo Ghati ni pamoja na kukashifu na kutoa tuhuma dhidi ya
kiongozi wa chama nje ya utaratibu na kuhujumu chama wakati wa
uchaguzi.
“Kwa
makosa hayo ambayo Leticia Ghati aliyatenda wakati wa Uchaguzi Mkuu wa
2015 Halmashauri Kuu ya Taifa, inamsimamisha uongozi na kumvua
uanachama,” alisema Mbatia.
Mustakabali wa chama
Akizungumzia mustakabali wa chama hicho katika Ukawa, Mbatia alisema Halmashauri Kuu ya chama hicho itaendelea kusimama imara kuhakikisha umoja huo unakuwa bora na taifa linapata Katiba kama yalivyokuwa malengo ya kuanzishwa kwake.
Akizungumzia mustakabali wa chama hicho katika Ukawa, Mbatia alisema Halmashauri Kuu ya chama hicho itaendelea kusimama imara kuhakikisha umoja huo unakuwa bora na taifa linapata Katiba kama yalivyokuwa malengo ya kuanzishwa kwake.
“NCCR
tutahakikisha Ukawa unaboreka na kusimama imara kwa ajili ya kupata
Katiba, tumeazimia kuunga mkono jitihada za kuunganisha vyama
vinavyounda umoja huu ili kufikia lengo la kuwa na chama kimoja cha siasa chenye nguvu,” alisema Mbatia.
Mbatia pia alizungumzia
hali ya kisiasa na kidemokrasia nchini na kusema chama chake kimebaini
kuwa taifa linaongozwa kwa matamko ya Rais John Magufuli badala ya
kufuata Katiba, sheria na kanuni.
Alisema demokrasia imeendelea kukiukwa
huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa na akatolea mfano
mwenendo wa Bunge ambao alisema licha ya kuwa chombo cha kikatiba chenye
mamlaka kamili ya kujiendesha, limeanza kuingiliwa katika uendeshaji
wake kwa wabunge kunyimwa fursa ya kujadili kwa uwazi masuala ya
Watanzania.
Alisema NCCR inakemea matu- mizi ya nguvu za dola kupitia
Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa,
kuwakamata na kuwaweka rumande viongozi wa kisiasa na kuwashtaki kwa
makosa mbalimbali.
“NCCR Mageuzi tunalaani tabia ya polisi kuwakamata na
kuwahoji mara kwa mara viongozi wa kisiasa na kuwashtaki kwa makosa
mbalimbali… vitendo hivi ni ukiukaji wa uhuru na haki za vyama vya siasa
katika kufanya kazi zao,” alisema Mbatia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni