Leo
July 27 2016 Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa imetoa hukumu ya
kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwanahabari wa kituo cha Television cha
chanel Ten, Daud Mwangosi.
Mahakama
hiyo imemuhukumu kwenda jela miaka 15 mshtakiwa wa mauaji hayo, askari
wa polisi kikosi cha kutuliza ghasia ‘FFU’ Pacificius Simon.
Hukumu
hiyo imekuja baada ya juzi mahakama hiyo kumkuta na hatia askari huyo
ya mauaji ya bila kukusudia ya Mwangosi yaliyofanyika September 2 2012
kwenye kijiji cha Nyololo, Mufindi wakatia CHADEMA ikifanya uzinduzi
wa matawi, huku kukiwa na katazo la mikutano au makusanyiko ya kisiasa
kutokana na seriakali kuongeza muda wa sensa ya watu na makazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni