BAADHI
ya mitambo, nguo na malighafi katika Kiwanda cha Nguo cha 21st Century
kilichopo Kihonda, Morogoro vimeteketea kwa moto na kusababisha hasara.
Akizungumzia
moto huo Clement Munisi, meneja uzalishaji wa kiwanda hicho amesema
kuwa, moto huo ulianza saa 12:00 asubuhi leo katika mashine moja ya
kuzalishia nguo kwa ulianza kwa kutoa cheche.
Amesema, wafanyakazi walijaribu kuuzima kwa kutumia kifaa maalumu cha kuzima moto (Fire extinguisher ) bila mafanikio yoyote.
Munisi
amesema kuwa, moto huo uliunguza baadhi ya mitambo na malighafi
zilizokuwa katika chumba kimoja ndani ya kiwanda hicho na kusababisha
hasara kubwa.
Amesema
kuwa, moto huo uliendelea kuenea katika vyumba vingine ndani ya kiwanda
hicho jambo ambalo lililosababisha baadhi ya nguo zilizokuwa
zikiendelea kutengenezwa kuungua. Hata hivyo, hajaeleza dhamani halisi
ya vitu vilivyoteketea kwa moto.
Ramadhani
Pilipili, Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Morogoro amesema
kuwa, licha ya kuwahi kufika mapema katika eneo la tukio na juhudi za
kuuzima moto, bado miundombinu ya kiwanda hicho imekuwa kikwazo.
“Miundombinu
ya kiwanda ni tatizo kutokana na kukosekana eneo sahihi la kupitishi
mipira ya maji na hivyo kulazimika kutumia muda mwingi kwa kuvunja ukuta
ili kufanikisha zoezi la uzimaji,” amesema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni