Na mwandishi
Teddy Thomas
Mtoto mmoja
wa ajabu amezaliwa katika hospital ya
Manyamanyama Wilayani Bunda Mkoani Mara
akiwa amekufa huku kiwiliwili cha mwili wake kikiwa kimetengana na kichwa.
Mtoto huyo alizaliwa
akiwa amekamilika sehemu mbalimbali za mwili wake isipokuwa kichwa chake
ambacho kilikuwa na muonekano tofauti mithili ya nyoka aina ya kobra.
Akielezea
tukio hilo baba wamtoto huyo Makoye Saguda alisema tatizo hilo lilianza usiku baada ya mkewe Tabu
Makoye kuanza kusumbuliwa na tumbo na
kuchukua hatua ya kwenda katika zahanati ya
kangetutya ambapo jitiahada za kumsaidia mama huyo hazikufanikiwa na
ndipo muuguzi katika zahanati hiyo akaamua kuwatuma katika Hospital ya
manyamanyama.
“Tatizo hili
lilianza usiku majira ya saa saba usiku wa kuamki juzi alipo niambia mkewangu
nikaamua kuchuku hatua ya kumpeleka
katika zahanati ya Kangetutya”alisema Makoye Saguda.
Makoye
aliezea jinsi alivyo sumbuliwa mkewe kwa maumivu makali wakati
wakujifungua kwani mtoto alitanguliza
miguu na mikono na kichwa kukatalia
ndani ya uzazi na baada ya muda kiwiwili
kilikatika na kutengana na kichwa hali iliyo pelekea kichwa hicho kubaki ndani ya uzazi wa mama
huyo kwa muda wa nusu saa.
Aliendelea
kueleza na kusema kwamba baada ya kichwa hicho kubaki ndani ya uzazi wa mama
huyo alimuaomba muuguzi apumzike akidai kwamba nguvu zimemuishia na amechoka
kusukuma ndipo muuguzi naye akaamua kumuacha kwa muda ili apumzike na aweze kupata
nguvu za kusukuma kile kichwa kilicho kuwa kimebaki ndani ya uzazi, lakini
baada ya muda mfupi mama huyo alihisi kupata nguvu za kusukuma na kichwa kile kikawa kimetoka.
“Chakushangaza
kichwa kile kilipo toka kilikuwa cha maajabu maana kilikuwa kinafanana na nyoka
mithili ya kobra huku kikiwa na macho, masikio,pua,na mdomo kama kawaida ya
mwanadamu alivyo”alisema Makoye.
Aidha Makoye
alisema kuwa mtoto huyo amezaliwa akiwa ni jinsia ya kiume huku kiwiwili cha
mtoto marehemu kikiwa kiko kawaida kabisa isipo kuwa kichwa ndicho kilionyesha
kushangaza.
Naye Mganga
mkuu wa hospital hiyo Nikodemas Masosota alisema hali hiyo husababishwa na
kujaa kwa maji kwa mama mjamzito hali ambayo hupelekea kuzaliwa watoto kama
hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni