WATUHUMIWA wawili wa ujambazi waliokuwa wakihusishwa na mauaji ya
wauamini watatu katika Msikiti wa Rahman pamoja na unyang’aji katika
maduka ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money, Hamis Juma (38) mkazi wa
Nyegezi ametoroka akiwa chini ya ulinzi wa polisi na mwingine Mohamed
Bishof au Gunda Mika (31) amefariki dunia.
Mtuhumiwa huyo
anadaiwa kuwatoroka polisi Julai 3, mwaka huu majira ya saa 2:00 usiku
katika eneo la mlima wa Kiloreli Nyasaka katika Manispaa ya Ilemela.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, mtuhumiwa
huyo aliwatoroka askari wa upeleelzi ambao aliwapeleka katika mlima huo
kwenda kuwaonyesha maficho majambazi wenzake wanayotyatumia kujificha.
Alisema
baada kufika eneo hilo majambazi wenzake walishituka na kuanza kufyatua
risasi askari hao ambao walitaharuki na kisha kujibu mashambulizi hayo.
Msangi alieleza kuwa wakati majambazi na askari wakiendelea kujibizana
kwa kurushiana risasi mtuhumiwa huyo Juma alitumia mwanya huo kuwatoroka
polisi na kutokomea usiku huo.
Katika mapambano hayo askari
waliambulia kupata risasi iliyokuwa moja ikiwa kwenye chemba ya bunduki
hiyo moja aina ya Short Gun iliyokatwa mtutu na kitako chake wake ambayo
ilikuwa ikitumiwa na majambazi hao baada ya kuitupa na kutokomea ambapo
msako na juhudi kubwa zinafanyika za kumsaka mtuhumiwa huyo.
Aidha,
katika tukio jingine mtuhumiwa mwingine wa matukio hayo ya uporaji na
mauaji ya waumini wa dini ya Kiislamu, Mohamed Bishof au Gunda Mika (31)
shombe wa Kiarabu amefariki dunia kutoka na majeraha aliyoyapata baada
ya kuruka kutoka kwenye gari la polisi.
Mtuhumiwa huyo aliruka
kutoka ndani ya gari hilo katika eneo la Kiloreli Nyasaka kwa nia ya
kutoroka ambapo alianguka barabarani na kuumia kichwani na sehemu
mbalimbali za mwili wake na alifariki wakati akikimbizwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza ya sekou Toure kwa matibabu. Wakati
akijaribu kutoroka kwa kuruka kutoka kwenye gari la polisi na kuanguka
Mtuhumiwa
huyo katika mahojiano na polisi alikiri kufanya uhalifu wa unyang’anyi
wa kutumia silaha kwenye maduka ya kutoa huduma za kifedha pamoja na
mauaji n wakati anakamatwa alikutwa kakiwa na vifaa vay kielektroni
(electronic divice) alivyokuwa akivitumia kufanya uhalifu jijini na nje
ya Jiji la Mwanza
Pia alikutwa akiwa na kompyuta mpakato
waliyopora katika tukio la uporaji la Mei 5, mwaka huu huko Kishiri
Centre mali ya Phares Gabriel ambaye walimjeruhi mguuni kwa kumpiga
risasi na kupora kiasi cha fedha kisichojulikana.
Msangi alisema
kuwa jeshi hilo linaendelea na msako dhidi ya watuhumiwa wanaodaiwa
kuhusika katika matukio ya uporaji kwe nye maduka ya M-Pesa, TigoPesa na
Airtely Money na kuhakikisha wanatiwa mbaroni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni