Imeelezwa
kuwa kutumika kwa fedha za miradi
mbalimbali tofauti na vile ilivyopangwa matumizi yake yakufanikisha miradi hiyo
kukamilika nimoja ya sababu inayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi
na Taifa kwa ujumla katika nchi inayokuwa kiuchumi.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya suala la usimamizi mzuri wa miradi
ya maendeleo kwa wananchi mkuu wa wilaya
ya Bunda Lidya Bhumpilipili alisema kutumia fedha za miradi katika matumizi
mengine nikurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
“Jambo
la kutumia fedha za miradi katika matumizi mengine kwa maslahi yenu ya watu
binafisi nikurudisha nyuma maendeleo ya nchi” Alisema Bhupilipili
Bhupilipili
alisema nijambo la aibu kwa wazawa na wasimamizi wa miradi kutumia fedha za miradi katika mambo yao ambao
hayanatija kwa taifa huku wakifahamu mwenendo wanchi yao katika ukuwaji wa
kiuchumi.
Hata hivyo
Bhumpilipili alisema ni wakati sasa wakutambuwa kuwa sote ni sehemu ya ujenzi wa taifa na si mtu
mmoja katika kuhakikisha kuwa nchi inafikia hatua nzuri katika suala zima la kiuchumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni