Vijana wa
mji wa Bunda mkoani Mra wameaswa
kujituma kwa moyo mmoja katika kufanya
kazi kwa bidii kwa kipindi hiki cha awamu ya tano ili kuendelea kujenga taifa
lisilo kuwa na vijana tegemezi katika ujenzi wa taifa.
Hayo yalisemwa
na baadhi ya vijana wa mji wa Bunda wakati wakizungumza na wandishi wa habari juu ya mwenendo wa maisha yasasa kwa vijana jinsi yanavyokwenda kila kukicha.
Walisema kuwa
vijana walio wengi siku hizi wamejisahau
kujituma katika shughuli mbalimbali zinazowaingizia kipato kwa siku na badala
yake wamekuwa ni watu wakuwa vijiweni bila sababu za misingi.
“Siku
hizi vijana tumejisahau kuwa sisi ndio wenye nguvu na ndio viongozi wa badaye” walisema vijana
Walisema
licha ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kusema watu wafanyekazi kwa
nguvu zote lakini bado kuna baadhi hawaoni umuhimu wa jambo hilo hali ambayo
inasababisha waanze kuwa tegemezi licha ya kuwa na nguvu za kufanya kazi.
Katika hatua
nyingine vijana hao waligusia suala la
mavazi yanayovaliwa na vijana kwasasa jambo ambalo limekuwa kero kwa watu licha
watu kuongelea kila kukicha.
“Licha
ya wazazi wetu kupiga kelele kila kukicha lakini ngoma bado iko palepale maana
sie tunaona ndo muda wetu” walisema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni