Chama cha
walimu Tanzania CWT Wilaya ya Bunda Mkoani Mara kimeiomba serikali kusikia
kilio cha madai ya walimu walio simamia mtiahani wa darasa la nne mwaka
2015.
Akizungumza katika hafla fupi ya mkono wa kwa heri kwa
walimu wastaafu katika ofisi za chama hicho Mwenyekiti wa chama cha walimu
wilaya ya Bunda Mongson Kabeho alisema
kuwa walimu 814 wanaidai serikali
jumla ya fedha tasilimu Milioni arobaini
na tano na laki tatu( 45,300,000) hivyo
ni vyema serikali ikawalipa madai hayo.
“Jumla ya walimu 814 wanaidai
serikali jumla ya fedha tasilimu
Milioni arobaini na tano na laki
tatu( 45,300,000) ni vyema serikali ikawalipa “alisema kabeho
Lakini pia alisema
kuna Walimu ambao walifanya kazi kwa uadilifu na kujituma waliostaafu tangu mwaka jana mwezi wa sita lakini hadi sasa mafao yao bado
hajalipwa hali inayo pelekea kuishi maisha magumu kwa walimu hao ambapo hali hiyo inadhalilisha taaluma ya ualimu.
“kuna walimu walifanya kazi kwa uadilifu na kujituma waliostaafu tangu mwaka jana mwezi wa sita lakini hadi sasa tunavyozungumza
mafao yao bado hajalipwa” alisema kabeho
Naye kwa
upande wake katibu wa chama hicho
Kambula malaba aliwapongeza
wastaafu hao na kwamba wanapaswa kujivunia kwa hatua waliofikia kwani wengi wanatamani kufikia hatua hiyo.
“Niwapongeze tu wazee wangu kwa hatua hii kwani wengi
wanatamani wafikie lakini wanashindwa hivyo jivunieni nyie kustaafu”alisema
malaba
Katika hatua nyingine nao wastaafu walioagwa katika
hafla hiyo ambao walipewa mkono wa kwa heri kwa kuzawadia mabati 20 na fedha tasilimu elfu ishirini kwa
ajili ya usafiri amabapo waliahidi kuwa
mabalozi wema kwa walimu vijana walioko
kazini katika shule mbalimbali.
“Twendeni tukawe mabalozi wema
kwa walimu vijana walioko kazini katika kuwaelimisha mambo mbalimbali
yanayopaswa kuelimishana”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni