MAOFISA
Ugavi wanne wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kitengo cha Maafa), wamepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa
madai ya kuiba mali za ofisi hiyo zenye thamani ya Sh milioni 100.
Wakisomewa
hati ya mashtaka mbele ya Hakimu, Respicius Mwijage, Wakili wa
Serikali, Jackson Chidunda aliwataja washtakiwa hao, kuwa ni Ahmed
Yusuph(48) Ofisa ugavi, Martine Tyeah(31) Ofisa Ugavi Msaidizi, Mwahija
Kimata(55),Ofisa ugavi msaidizi na Halima Mwanjiro(33) Ofisa Ugavi.
Alidai
washtakiwa hao, wanadaiwa kati ya Aprili, 2014 na Septemba, mwaka huo
huo katika eneo la Keko lililopo karibu na Ofisi ya Bohari Kuu ya
Madawa(MSD), Temeke jijini Dar es Salaam, wakiwa waajiriwa wa Ofisi ya
Waziri Mkuu, wanadaiwa kuiba mabati 5074,Sufuria 200 na mikeka 348
vyenye thamani ya Sh 100,164,000.
Alidai
mali hizo zinamilikiwana Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa ambazo
zilitolewa kwa ajili ya maafa kupitia kitengo hicho, lakini washtakiwa
hao wanadaiwa kuchukua kinyume cha sheria.
Alidai upelelezi wa shauri hilo,bado haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hata
hivyo, Hakimu Mwijage aliwataka kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja
ambaye atasaini bondi ya Sh milioni 25 ambapo washtakiwa hao walikidhi
mashart hayo na kuachiliwa kwa dhamana.
Shauri hilo, limeahirishwa hadi Agosti 22, litakapotajwa tena.
Wakati
huo huo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempandisha kizimbani raia wa
China, Senxin Van baada ya kubainika kufanya kazi kinyume na kibali
chake.
Akisomewa
hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Huruma Shahidi, Wakili wa Serikali,
Novatus Mlay alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Julai, 12,
mwaka huu katika kampuni ya uwekezaji ya Tenglong iliyopo Kinondoni
jijini Dar es Salaam ambapo aliajiriwa kama daktari wakati kibali chake
kinamruhusu kufanya kazi katika kampuni ya kutengeneza viatu ya Tong
Xing kama Mkurugenzi.
Katika utetezi wake, mshtakiwa huyo aliiomba mahakama hiyo kumsamehe kwa sababu ni babu mwenye wajukuu na mlezi wa familia na kwamba katika kampuni hiyo ni Mkurugenzi ambaye ameajiri watanzania wengi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni