Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP
Ernest Mangu ametuma timu ya Maofisa wa Polisi ikiongozwa na Kamishna wa
Polisi Jamii Mussa Alli Mussa kwenda Zanzibar kushughulikia kero na malalamiko
ya wananchi juu ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili kwa watoto/wanawake
ambavyo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.
Timu hiyo imepewa jukumu la
kuchunguza vitendo hivyo vya udhalilishaji na kiini chake na hatimaye kuja na
mpango mkakati wa kuzuia vitendo hivyo ikiwemo kuwakamata wahusika na
kuwafikisha mahakamani.
IGP Mangu amewataka wananchi wa
Zanzibar, Taasisi za kiserikali na Taasisi za kiraia zilizopo Zanzibar kutoa
ushirikiano kwa timu hiyo ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na
maadili ya Watanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni