Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya
linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kufukua kaburi la marehemu ambaye likuwa
ni mlemavu wa ngozi (Albino) aliyefariki mwaka 2010 kwa lengo la kuchukua
viungo vyake.
Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa na
Kamanda a Polisi Mkoani Mbeya DCP Dhahiri Kidavashari inasema kuwa mnamo tarehe
03.01.2017 majira ya saa 01:00 usiku katika Kijiji cha Mumba kilichopo Kata ya
Ilembo, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JONAS JOHN mkazi wa Chapakazi
alikamatwa na askari Polisi akiwa na wenzake wawili wakifukua kaburi la
marehemu SISTER OSISARA aliyekuwa mlemavu wa ngozi (ALBINO)
Inadaiwa kuwa marehemu alifariki
dunia mwaka 2010 kwa ugonjwa wa homa na kuzikwa katika makaburi ya Kijiji cha
Mumba.
Mtuhumiwa alikutwa na majembe na
makoleo ambayo walikuwa wakiyatumia kufukuria kaburi hilo. Baada ya mahojiano
mtuhumwa huyo aliwataja washirika wenzake wawili ambao walikimbia baada ya
kuwaona askari.
Jeshi hilo linaendelea na msako
mkali wa kuwatafuta watuhumiwa .
Katika tukio lingine Mnamo tarehe
03.01.2017 majira ya saa 3:30 usiku katika kata ya Makongolosi wilayani Chunya,
mkoa wa Mbeya, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la KELVIN KUBANDA mkazi wa
Kahama alikamatwa akiwa na bhangi kete 10 sawa na uzito wa gramu 55.
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa katika
kijiwe cha kuvutia Bhangi. Upelelezi unaendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni