Shirika la masoko ya kariakoo limewasimamisha kazi maafisa wawili wa
idara ya manunuzi kwa tuhuma za kufanya manunuzi kinyume cha sheria ya
manunuzi.
Shirika la masoko ya Kariakoo limewasimamisha kazi maafisa wawili wa
idara ya manunuzi kwa tuhuma za kufanya manunuzi kinyume cha sheria ya
manunuzi.
Meneja Mkuu wa Shirika hilo HETSON KIPSI amewataja waliosimamishwa
kazi ni mkuu wa kitengo cha manunuzi wa shirika hilo MATHIAS MBAFU na
msaidizi wake HENRIKA KAWILI .
KIPSI amesema maafisa hao wanatuhumiwa kughushi saini ya meneja mkuu
ili waweze kununua mafuta ya jenereta na vifaa vingine na uchunguzi wa
tuhuma hizo unaendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni