Mkuu wa mkoa wa ARUSHA, MRISHO GAMBO amemwagiza Mkuu wa wilaya ya ARUSHA
kuunda timu ya kufuatilia fedha za mikopo zinazotolewa na halmashauri
kwa ajili ya Vijana na Wanawake kwa kipindi cha miaka MITATU namna
zilivyotumika.
Mkuu wa mkoa wa ARUSHA, MRISHO GAMBO amemwagiza Mkuu wa wilaya ya
ARUSHA kuunda timu ya kufuatilia fedha za mikopo zinazotolewa na
halmashauri kwa ajili ya Vijana na Wanawake kwa kipindi cha miaka MITATU
namna zilivyotumika.
GAMBO ametoa agizo hilo jijini ARUSHA wakati akikabidhi mfano wahundi yenye thamani ya shilingi Milioni 425 kwa vikundi vya wanawake 85 na hundi ya shilingi Milioni 199 kwaajili ya vikundi 40 vya vijana wa jiji hilo,GAMBO nakusisitiza kuwa fedha hizo zinatakiwa zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa ya kufanya shughuli za kiujasiriamali.
Amesema bado jiji hilo linatoa fedha kidogo ikilinganishwa na mapato yanayokusanywa na kuvinufaisha vikundi vya vijana na wanawake hivyo ni vyema mikopo iliyotolewa ikadhibitiwa ikiwa nipamoja na kufanya uchunguzi wa fedha za mikopo zilizotolewa katika kipindi cha miaka MITATU.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii katika jiji la ARUSHA, JANETH MMASI, amesema mikopo hiyo itasaidia vikundi 125 vya Vijana na Wanawake katika kujikwamua kiuchumi huku Mkuu wa wilaya ya ARUSHA, GABRIEL DAQQARO akiahidi kusimamia kikamilifu fedha hizo ili zitumike kama ilivyokusudiwa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni