Mbunge
wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi.
Wakili
wa Serikali Kishenyi Mutalemwa aliwasilisha maombi ya kupinga dhamana
yaTundu Lissu kwa madai kwamba amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani
si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa
maneno ya uchochezi.
Hakimu Huruma Shaidi, ametupilia mbali ombi hilo la serikali na kumpa Tundu Lissu dhamana ya sh. Milioni 20
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni