Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, leo
imeshindwa kusikiliza rufani ya Jamhuri dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema kupinga dhamana yake, baada ya mawakili wa Serikali kuwasilisha
notisi ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa wakipinga kusikilizwa kwa
rufani hiyo .
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya
Arusha, Salma Maghimbi alitarajiwa kutoa uamuzi juu ya rufaa ya
Jamhuri iliyopinga Lema kupatiwa dhamana Novemba 11 na Hakimu Mkazi wa
Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha katika kesi namba 440 na 441/2016
ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, ambapo siku hiyo
Jamhuri iliwasilisha notisi ya mdomo.
Baada ya Lema kufikishwa mahakamani
saa 3.25 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali, huku pia polisi wakiwa wametanda
viwanja vya Mahakama Kuu ndani na nje sanjari na gari moja la maji ya kuwasha,
baada ya mawakili wa pande zote kujitambulisha Jaji Maghimbi alisoma
notisi ya Jamhuri kupeleka shauri hilo Mahakama ya Rufaa na kueleza kufungwa
kisheria kutoa uamuzi wa rufani hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni