Wakazi wa kijiji cha, ITENKA katika Halmashauri ya NSIMBO Wilayani
MPANDA Mkoani KATAVI wameiomba serikali kuwaruhusu kutumia miundombinu
ya umwagiliaji wa kienyeji wakati wakisubiri kuwekewa miundombinu ya
kisasa katika bonde la umwagiliaji la ITENKA.

Wakazi hao wametoa ombi hilo wakati wa mkutano wa hadhara uliokua na
lengo la kujadili shughuli za maendeleo katika jimbo la NSIMBO, mkutano
ulioongozwa na Mbunge wa jimbo hilo RICHARD MBOGO.
Wakazi hao Wamesema wao wanategemea kilimo cha mpunga hivyo
kubomolewa kwa miundo mbinu iliyokuwa imejengwa na kuzuia maji
kutiririka katika bonde la mto katuma kumeyafanya Maisha yao kuwa
mashakani kwa kuwa hawana tegemeo jingine la uchumi tofauti na kilimo
cha mpunga katika bonde hilo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la NSIMBO Richard Mbogo amesema
atawasilisha suala hilo serikalini ili liweze kufanyiwa kazi na
kuwataka Wakazi hao kuheshimu sheria za uhifadhi wa mazingira kwa kutii
maagizo yaliyotolewa na serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni