Mkoa wa Mara umegundulika kuwa chini
ya viwango vizuri vya kitaifa vya upatikanaji vya huduma ya maji safi na salama kwa wananchi
jambo ambalo linatajwa kuwa moja ya sababu inayopelekea magonjwa ya mripuko kutokea
katika mkoa huo.
Hayo yalisemwa na mkuu wa Mkoa wa
Mara dk.Charles Mulingwa wakati akizungumza na watumishi wa serikali pamoja na
madiwani wa halmashauri zote mbili ya mji wa Bunda na Halmashauri ya Wilaya ya
Bunda katika ukumbi wa mikutano mjini Bunda.
Mulingwa alisema kuwa bila kujali
mijini au vijijini katika suala la maji safi na salama kwa wastani ni asilimia 53 licha ya kuwa na
vyanzo vingi vya maji ambavyo vingesaidia upatikanaji wa maji safi na salama
kwa wananchi.
“Ni sema bila kujali kuwa
mjini au kijijini hali hii ya kutopatikana kwa maji safi na salama ipo asilimia
53% tu” alisema
Mulingwa
Naye mkuu wa wilaya ya Bunda Lydia
Bupilipili alitumia fulsa hiyo kumuomba mkuu wa Mkoa kusaidia kusukuma suala la
kuhamishwa kwa makao makuu ya hifadhi ya mbunga ya wanyama Serengeti Nation park kuhamishiwa mjini Bunda
ili kusaidia huduma zingine kusonga mbele.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni