Wauguzi na
Manesi katika kituo cha Afya cha Kasahunga wilaya ya bunda mkoani Mara wametakiwa
kuwa na moyo wa huruma kwa wagonjwa huku wakisisitizwa kuacha kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa ili kuzuia
vifo visivyo tarajiwa hasa kwa mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka
mitano.
Kiongozi wa
mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu George Jackson Mbijima aliyasema hayo
wakati akizinduwa jengo la upasuaji katika kituo cha Afya cha
Kasaunga kilichopo wilayani Bunda.
“Madaktari,manesi
na wauguzi jengo hili ni zuri pamoja na vifaa vyake vizuri litakuwa na thamani kubwa kama huduma itatolewa kwa ubora ambao
utaendana na jengo lenyewe “alisema Mbijima
Aidha Kiongozi
huyo aliwataka wanachi wa eneo hilo kuwa na ushirikiano na madaktari pamoja na
manesi ili huduma inato lewa iwe bora na
yenye uhakika kwa wagonjwa.
Akisoma taarifa mmoja wa wauguzi wa
kituo hicho kwa ya mgaga mkuu mfawidhi Dk. Malima Kawawa alisema Jengo hilo
limegharimu shilingi milioni mia tano arubaini na moja mia saba therasini Elfu
mia nane hamsini na tano(541,730,855)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni