Serikali imeombwa kuangalia uwezekano wa kuipatia halmashauri ya
wilaya ya Bunda mkoani Mara gari la wagonjwa haraka iwezekanavyo hali
itakayosaidia kuboresha kwa huduma ya afya wilayani humo.
Mganga mkuu wa halmashauri hiyo,Dk.Jonathan Budemu aliwasilisha
ombi katika taarifa yake aliyoitoa kwa mkuu wa wilaya hiyo,Lydia Bupilipili
akisema kukosekana kwa gari hilo kumezorotesha kwa kiwango kikubwa huduma ya
afya.
Dk.Budemu aliyemwomba mkuu huyo wa wilaya kusaidia kusukuma
kufanikiwa kwa ombi hilo, amesema kutokana na hali hiyo wamekuwa wakishindwa
kuwasafirisha kwa wakati wagonjwa mahututi kuwapeleka kwenye matibabu zaidi.
Kwa upande wake Bupilipili licha ya kukubali kusukuma
utekelezwaji wa ombi hilo lakini pia aliwataka watumishi wa idara ya afya
kufanya kazi zao kwa uadilifu wakizingatia kwamba wanashughulika na maisha ya
watu huku akionya kutosita kumwadhibu kisheria mzembe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni