Jumanne, 5 Julai 2016

Mtuhumiwa wa ujambazi na mauaji msikitini Mwanza atoroka


WATUHUMIWA wawili wa ujambazi waliokuwa wakihusishwa na mauaji ya wauamini watatu katika Msikiti wa Rahman pamoja na unyang’aji katika maduka ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money, Hamis Juma (38) mkazi wa Nyegezi ametoroka akiwa chini ya ulinzi wa polisi na mwingine Mohamed Bishof au Gunda Mika (31) amefariki dunia.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwatoroka polisi Julai 3, mwaka huu majira ya saa 2:00 usiku katika eneo la mlima wa Kiloreli Nyasaka katika Manispaa ya Ilemela.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, mtuhumiwa huyo aliwatoroka askari wa upeleelzi ambao aliwapeleka katika mlima huo kwenda kuwaonyesha maficho majambazi wenzake wanayotyatumia kujificha.

Alisema baada kufika eneo hilo majambazi wenzake walishituka na kuanza kufyatua risasi askari hao ambao walitaharuki na kisha kujibu mashambulizi hayo. Msangi alieleza kuwa wakati majambazi na askari wakiendelea kujibizana kwa kurushiana risasi mtuhumiwa huyo Juma alitumia mwanya huo kuwatoroka polisi na kutokomea usiku huo.

Katika mapambano hayo askari waliambulia kupata risasi iliyokuwa moja ikiwa kwenye chemba ya bunduki hiyo moja aina ya Short Gun iliyokatwa mtutu na kitako chake wake ambayo ilikuwa ikitumiwa na majambazi hao baada ya kuitupa na kutokomea ambapo msako na juhudi kubwa zinafanyika za kumsaka mtuhumiwa huyo.

Aidha, katika tukio jingine mtuhumiwa mwingine wa matukio hayo ya uporaji na mauaji ya waumini wa dini ya Kiislamu, Mohamed Bishof au Gunda Mika (31) shombe wa Kiarabu amefariki dunia kutoka na majeraha aliyoyapata baada ya kuruka kutoka kwenye gari la polisi.

Mtuhumiwa huyo aliruka kutoka ndani ya gari hilo katika eneo la Kiloreli Nyasaka kwa nia ya kutoroka ambapo alianguka barabarani na kuumia kichwani na sehemu mbalimbali za mwili wake na alifariki wakati akikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza ya sekou Toure kwa matibabu. Wakati akijaribu kutoroka kwa kuruka kutoka kwenye gari la polisi na kuanguka

Mtuhumiwa huyo katika mahojiano na polisi alikiri kufanya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha kwenye maduka ya kutoa huduma za kifedha pamoja na mauaji n wakati anakamatwa alikutwa kakiwa na vifaa vay kielektroni (electronic divice) alivyokuwa akivitumia kufanya uhalifu jijini na nje ya Jiji la Mwanza

Pia alikutwa akiwa na kompyuta mpakato waliyopora katika tukio la uporaji la Mei 5, mwaka huu huko Kishiri Centre mali ya Phares Gabriel ambaye walimjeruhi mguuni kwa kumpiga risasi na kupora kiasi cha fedha kisichojulikana.

Msangi alisema kuwa jeshi hilo linaendelea na msako dhidi ya watuhumiwa wanaodaiwa kuhusika katika matukio ya uporaji kwe nye maduka ya M-Pesa, TigoPesa na Airtely Money na kuhakikisha wanatiwa mbaroni.




Watumishi wilayani Bunda watakiwa kufanya kazi kwa kusoma majira na nyakati.


Mkuu wa  wilaya ya Bunda Lidya Simeon Bhupilipili amewataka watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda na halmashauri ya mji  kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma na kusoma majira na nyakati katika utendaji wao wa kazi
Hayo aliyasema wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo katika ukumbi wa halmashauri ya bunda baada ya kufanya makabidhiano na aliye kuwa mkuu wa wilaya hiyo Joshua Chacha Mirumbe.
Fanyeni kazi kwa kujituma na kusoma majira na nyakati katika utendaji wenu wa kazi
Bhupilipili alisema kuwa watumishi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa kujiamini  bila kuwa na woga wala hofu kwa kufuata na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi CCM.
Kwa sasa tunaendesha serikali kwa kufuata ilani ya ccm na si vinginevyo
Aidha aliwaomba watumishi kuwa na  ushirikiano katika utendaji kazi wao ili waweze kuleta maendeleo katika wilaya ya Bunda na Taifa kwa ujumla huku akiwaonya  watumishi kuacha  utumiaji mbaya wa fedha na uandaaji wa  taarifa zisizo za kweli katika miradi  mbalimbali ya maendeleo kwa Wananchi.
Ni wambie tu kwa wale wapenda kuchakachua taarifa na utumiaji wa fedha vibaya niwape onyo tu kuwa acheni tabia hiyo
Awali mkuu wa wilaya mstaafu  Joshua cha cha Mirumbe aliwaomba watumishi wa halmashauri zote mbili kuonesha ushirikiano wa dhati kwa mkuu wa wilaya mpya   Bhupilipili katika kuleta maendeleo ya wananchi.
Ni waombe watumishi mshirikiane vizuri na mkuu huyu wa wilaya katika mambo ya maendeleo ya wananchi na kwa taifa kwa ujumla























Jumapili, 3 Julai 2016

Ukistajabu ya Musa utayaona ya Filauni Mtoto wa maajabu azaliwa katika hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda.






 Na mwandishi Teddy Thomas

Mtoto mmoja wa ajabu  amezaliwa katika hospital ya Manyamanyama  Wilayani Bunda Mkoani Mara akiwa amekufa huku kiwiliwili cha mwili wake kikiwa kimetengana na kichwa.

Mtoto huyo alizaliwa akiwa amekamilika sehemu mbalimbali za mwili wake isipokuwa kichwa chake ambacho kilikuwa na muonekano tofauti mithili ya nyoka aina ya kobra.

Akielezea tukio hilo baba wamtoto huyo Makoye Saguda alisema tatizo hilo  lilianza usiku baada ya mkewe Tabu Makoye  kuanza kusumbuliwa na tumbo na kuchukua hatua ya kwenda katika zahanati ya  kangetutya ambapo jitiahada za kumsaidia mama huyo hazikufanikiwa na ndipo muuguzi katika zahanati hiyo akaamua kuwatuma katika Hospital ya manyamanyama.

“Tatizo hili lilianza usiku majira ya saa saba usiku wa kuamki juzi alipo niambia mkewangu nikaamua kuchuku  hatua ya kumpeleka katika zahanati ya Kangetutya”alisema Makoye Saguda.

Makoye aliezea jinsi alivyo sumbuliwa mkewe kwa maumivu makali wakati wakujifungua   kwani mtoto alitanguliza miguu  na mikono na kichwa kukatalia ndani ya uzazi  na baada ya muda kiwiwili kilikatika na kutengana na kichwa hali iliyo pelekea  kichwa hicho kubaki ndani ya uzazi wa mama huyo kwa muda wa nusu saa.

Aliendelea kueleza na kusema kwamba baada ya kichwa hicho kubaki ndani ya uzazi wa mama huyo alimuaomba muuguzi apumzike akidai kwamba nguvu zimemuishia na amechoka kusukuma ndipo muuguzi naye akaamua kumuacha kwa muda ili apumzike na aweze kupata nguvu za kusukuma kile kichwa kilicho kuwa kimebaki ndani ya uzazi, lakini baada ya muda mfupi mama huyo alihisi kupata nguvu za kusukuma  na kichwa kile kikawa kimetoka.

“Chakushangaza kichwa kile kilipo toka kilikuwa cha maajabu maana kilikuwa kinafanana na nyoka mithili ya kobra huku kikiwa na macho, masikio,pua,na mdomo kama kawaida ya mwanadamu alivyo”alisema Makoye.

Aidha Makoye alisema kuwa mtoto huyo amezaliwa akiwa ni jinsia ya kiume huku kiwiwili cha mtoto marehemu kikiwa kiko kawaida kabisa isipo kuwa kichwa ndicho kilionyesha kushangaza.


Naye Mganga mkuu wa hospital hiyo Nikodemas Masosota alisema hali hiyo husababishwa na kujaa kwa maji kwa mama mjamzito hali ambayo hupelekea kuzaliwa watoto kama hao.






Jumatano, 29 Juni 2016

Tundu Lissu Awekwa Rumande Kwa Kukosa Dhamana.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana, mara baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kufuatia kauli yake aliyoitoa jana inayoelezwa kuwa si ya kiungwana.

Mbunge huyo amehojiwa kwa saa tatu  kuhusiana na maneno mengine ambayo anadaiwa kuyaandika kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni ya uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kuwa Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana na hataachiwa leo, hivyo atalala huko mpaka kesho.

Alichokiandika Rais Magufuli kuhusu ugunduzi wa gesi ya Helium nchini Tanzania

Jana ziliripotiwa taarifa kuwa watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalamu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.

Leo June 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kupitia account yake ya twitter amepost akizungumzia ugunduzi huo huku akitoa wito kujipanga katika eneo la mikataba.

"Tunamshukuru Mungu Tanzania tumegundua gesi aina ya Helium(He),wito wangu kwa wachumi,wanasheria na watanzania wote kwa ujumla tujipange

"Ugunduzi huu utuelekeze kujipanga hasa ktk eneo la mikataba yetu ili rasilimali hii adimu isaidie kuujenga uchumi wetu"

Mfuko wa jimbo la Bunda mjini waweka hadharani



Mfuko wa jimbo la Bunda Mjini halmashauri ya mji Bunda mkoani Mara umetumia zaidi ya sh.milioni 25 katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo jimboni humo katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu.

Katibu wa mbunge wa jimbo hilo,Kaunya Yohana alisema kuwa miradi iliyopewa kipaumbele katika kipindi hicho ni ya elimu,afya,maji na utawala ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hizo kwa ukaribu.

Alifafanua kuwa shughuli zilizofanyika ni kuezeka vyumba vya madarasa na kuchimba choo katika shule za msingi za Kunzugu,Kitaramaka,Nyerere,Bigutu na Bushigwamara pamoja na kununua madawati katika shule hizo.

Aidha Kaunya alisema pia kwamba fedha hizo zimechimba kisima na kukarabati tenki la maji katika vijiji vya Misisi na Mihale pamoja na kujenga ofisi ya serikali ya kijiji cha Rwabu na kutoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana na mbunge wa jimbo hilo,Esta Bulaya ili wafikie maendeleo yaliyokusudiwa.

Mahakama Kuu Arusha Yatengua ushindi wa Mbunge wa Longido, Onesmo Ole Nangole (CHADEMA), yaamuru kurudiwa uchaguzi katika jimbo hilo.

Kesi iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika mahakam kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii

Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dr KIRUSWA alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya mbunge wa Longido mh ONESMO NANGOLE

Akisoma hukumu hiyo,Jaji MWAGESI alisema kwamba mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.

Katika shauri hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni
1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole
3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura
4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.
5.kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo

Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;
 
Kutokana na kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa sheria,Natamka kwamba;

Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa kujirisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki."