Redio Mazingira Fm sauti ya jamii iliyopo
katika Mji Wwa Bunda Mkoani Mara Kupitia kipindi cha Duru za Habari(DZH) kinachoendeshwa
na Thomas J Masalu na Andrew Mbwiga kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa kumi
na mbili jioni katika cha kipengele cha Kubwa la leo siku ya jana walikusogezea
habari kuhusu Shirika la umeme Tanzania Tanesco wilaya ya Bunda Mkoa Mara, kuwa
wametekeleza agizo lililoagizwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt
John Magufuli la kusitisha huduma ya umeme kwa wale wote wanaodaiwa.
Kaimu meneja wa tanesco wilayani
hapo bwana Yusuph Mbaa alisema wametekeleza agizo hilo kwa kuanza kuwakatia
umeme mamlaka ya maji wilaya ya bunda kwa kushindwa kulipa deni wanalodaiwa zaidi ya shilingi milioni 200.
Aliiambia Mazingira fm kwamba
kufikia hatua ya kukata umeme kwa mamlaka ya maji inatokana na deni la muda
mrefu na tayari walikwishapewa notisi ya kutakiwa kulipa deni hilo lakini
hawakutekeleza, na kuongeza kuwa wadaiwa wengine pia wameshapatiwa taarifa ya
kutakiwa kulipa madeni yao kwani Tanesco bado wako katika hatua ya kutekeleza
agizo la Rais ili shirika lijiendeshe.
Hata hivyo bwana mbaa aliwataka
wateja wengine wanaodaiwa na hawajalipa kulipa madeni hayo ili kuepukana na
usumbufu wanaoweza kuupata pindi watakapokatiwa umeme.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni