Mkurugenzi wa
halmashauri ya mji wa bunda janeth mayanga , aliyekuwa mgeni rasmi kwa
niaba ya mkuu wa wilaya bi lydia bupilipili katika uzinduzi wa kampuni ya sola ya sunking
amesema kuwa ujio wa kampuni hiyo itasaidia ongezeko la fursa za
ajira kwa jamii katika mji wa
bunda na mkoa wa mara kwa ujumla .
Kufuatia uzinduzi huo Mayanja
amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kununua mitambo ya sola kutoka katika kampuni hiyo kwa
kuwa ina sola nzuri na inayokidhi mahitaji ya watumiaji wake.
Aidha Mayanja
amewakumbusha mawakala wa kampuni hiyo kufuata sheria ya vibali na kulipa kodi
ili serikali iweze kujipatia mapato.
Kwa upande wake afisa
biashara wa kampuni hiyo bi Jodie Wu
amesema kuwa bidhaa hiyo imesambazwa katika wilaya tano za mkoa wa mara ikiwemo Rorya, Tarime,
Butiama, Bunda na Serengeti ambapo kwa sasa ina jumla ya mawakala
50.
Hata hivyo bi wu amesema kuwa Nia ya Sunking ni kuhakikisha wananchi wa
maisha ya chini wanaishi kama matajiri, kwani wameamua kuwaletea mwanga mzuri
kwa bei ya chini kabisa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni