Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imesema kuwa haihusiki kumtafutia mnufaika wa mkopo ajira badala yake inahusika kumpatia mwanafunzi mkopo na akishamaliza muda wa masomo atatakiwa kurejesha mkopo wake.
Hayo yamesemwa jana
Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na
Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisobwa
wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia kipengele cha Kikaango cha EATV.
“Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatoa mikopo suala la kutafuta ajira
halituhusu hivyo mnufaika yoyote asiwe na kigezo kwamba hajapata kazi ,
hiyo siyo kazi yetu, kazi yetu ni kuwawezesha kupata elimu basi” Alisema Mwaisobwa.
Aidha Mwaisobwa alisema
wanufaika wote ambao walipata mikopo wanatakiwa kukatwa asilimia 8% ya
pato la mwezi, na kama mtu anafanya kazi binafsi na hakatwi popote
atatakiwa kutoa kiwango cha 120,000/= na kwa ambao wamenufaika na
hawataki kuanza kulipa mkopo watapigwa penati ya 10% ya mkopo kwa mwaka.
Pamoja
na hayo Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imewataka walioomba mikopo
kuvuta subira kwani Bodi inasubiri majina kutoka Tume ya Vyuo Vikuu ili
Bodi ya Mikopo iweze kufahamu vyuo walivyopangiwa na kiwango cha ada ili
haki iweze kutendeka kwa waombaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni