Alhamisi, 9 Februari 2017

WATUHUMIWA 17 WA DAWA ZA KULEVYA WAKAMATWA SHINYANGA…MAJINA MENGINE ZAIDI YA 20 YAPO KWA DC SHINYANGA

Na mwandishi wetu 
Vita dhidi ya dawa za kulevya imetua mkoani Shinyanga ambapo jumla ya watu 17 wanaotuhumiwa kuwa ni watumiaji wa dawa hizo ikiwemo unga na mirungi wanashikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo amesema mbali na watu 17 kushikiliwa na polisi pia ofisi yake imepokea majina zaidi ya 20 ya watu wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya. 

“Mheshimiwa rais ametangaza kuwa hii ni vita ya nchi nzima,baada ya wananchi kusikia vita ya dawa za kulevya ikiendelea mkoani Dar es salaam,wametuletea majina zaidi ya 20 ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya,wanasema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kupiga vita dawa hizi”,amesema Matiro. 

“Wananchi wenyewe kwa moyo mweupe kabisa ndiyo wametuletea majina ya watu wanaotumia na kuuza dawa za kulevya ikiwemo unga na mirungi,kamati ya ulinzi na usalama tumeunda kikosi kazi cha kushughulikia majina yanayoletwa ili kubaini kama ni kweli wanajihusisha na dawa za kulevya”,alisema Matiro. 

Ametumia fursa hiyo kulipongeza jeshi la polisi kwa jitihada zake dhidi ya dawa za kulevya na kufanikisha kukamata watuhumiwa 17 huku akikisisitiza kuwa vita hiyo siyo ya Dar es salaam pekee bali inatakiwa kufanyika nchi nzima kwani watumiaji na wauzaji wa dawa hizo wapo kila mahali nchini. 

TCRA YAZIPIGA PINI MICHUZI TV, AYO TV NA GLOBAL TV, YAANDAA KANUNI ZA USAJILI WA TV MTANDAO ZOTE

Na mwandishi wetu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Michuzi TV,
AYO TV na Global TV kusitisha huduma zao za TV mtandaoni hadi hapo kanuni za usajili rasmi ambazo mamlaka hiyo imesema inaandaa  kwa
huduma hizo zitapokuwa tayari.
Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi James
Kilaba tarehe 30 January mwaka huu, imevitaka vyombo hivyo ambavyo vinapendwa
sana nchini na nje ya nchi kuacha mara moja kutoa huduma za TV mtandaoni.
“Kwa mujibu wa section 13 (1) of the electronic and
postal communications Act Cap 306, sheria za Tanzania zinahitaji watoa huduma
zozote za aina hiyo wanahitaji leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano”,
imesema barua hiyo.
Wamiliki wa mitandao hiyo – Millard Ayo, Ankal Issa Michuzi
na Abdallah Mrisho –  wameeleza
kushtushwa kwao kwa agizo hilo la ghafla, tena wakati hata kanuni zenyewe hazijawekwa.
              
“Gloval
TV ipo tayari hata leo kukamilisha taratibu za usajili – kama zingekuwepo – na
kwa sababu bado kukamilika tunaomba kupewa muda zaidi chini ya uangalizi wakati
tunasubiria kanuni hizo mpya,” alisema Abdallah Mrisho, Meneja Mkuu wa
Global Publishers.
Ankal Michuzi na Millard  Ayo waliunga mkono kauli hiyo na kwa pamoja
watatu hao wameomba kuonana na mkurugenzi wa TCRA ili kuwasilisha maombi rasmi
ya kuruhisiwa kuendelea kutoa huduma hiyo kwa muda wakati kanuni zikisubiriwa. 
Bahati mbaya Mhandisi Kilaba alikuwa safari na swala hilo limepangwa
kushughuliwa ataporejea wiki ijayo.
“Ukizingatia kwamba tumekuwa tunatoa huduma hii kwa muda mrefu na haijulikani kanuni zitakuwa tayari lini tunaomba TCRA iangalie namna ya kufanya ili wananchi wanaotutegemea sana wasikose huduma hii”, alisema Ankal. Hata hivyo vituo hivyo vitatu vinaendelea kuhudumu nje ya mchakato wa TV mtandao.
Ayo TV, Michuzi TV na Global TV,  ambazo zinaongoza kwa mbali kwa kutazamwa na
watu wengi nchini na nje ya nchi, ni TV mtandao pekee zilizoitikia mwito wa
TCRA, kati ya vituo mtandao  takriban 51
vilivyopata barua hiyo.

Mahakama Yatupilia Mbali Pingamizi la Serikali......Yampa Tundu Lissu DHAMANA Ya Milioni 20



Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi.

Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa  aliwasilisha maombi ya kupinga dhamana yaTundu Lissu kwa madai kwamba   amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi.

Hakimu Huruma Shaidi, ametupilia mbali ombi hilo la serikali na kumpa  Tundu Lissu dhamana ya sh. Milioni 20